LONDON:Mwanaharakati wa kiislamu ashtakiwa London | Habari za Ulimwengu | DW | 30.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON:Mwanaharakati wa kiislamu ashtakiwa London

Mwanaharakati wa kidini Abu Izadeen aliyena msimamo mkali wa dini ya kiislamu na ambaye anaikosoa mara kwa mara serikali ya Tony Blair kwa kuwadhalilisha waislamu ameshtakiwa pamoja na wenzake watano kwa madai ya kuchochea ugaidi nchi za nje pamoja na kufadhili shughuli za kigaidi.

Izadeen mwenye umri wa miaka 32 na wenzake wameshtakiwa kufuatia kukamatwa kwao katika msako mkali wa kupambana na ugaidi ulioendeshwa katika mji wa London jumaane iliyopita na watafikishwa mbele ya mahakama ya Westminster hii leo.

Hatua ya kukamatwa kwa Izadeen imechukuliwa mwaka mmoja baada ya kumkaripia na kumfedhehesha waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza John Reid wakati alipokuwa akihutubia katika kituo cha kiislamu kwenye mji wa East London.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com