1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:John Reid waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza kuacha wadhifa wake Juni

6 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC4M

Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza John Reid ametangaza kumuunga mkono waziri wa fedha Gordon Brown kuwa waziri mkuu mpya wa nchi hiyo.

Tangazo hilo limemaliza uvumi juu ya uwezekano wa John Reid kutaka kugombea nafasi hiyo.

Mwanasiasa huyo mwenye usemi mkubwa nchini Uingereza pia amesema ataachia wadhifa wake wa waziri wa mambo ya ndani mnamo mwisho wa mwezi juni.

Waziri mkuu Tony Blair anatarajiwa wiki ijayo kutangaza ratiba ya kuondoka kwake madarakani baada ya kuingoza Uingereza kwa kwa miaka 10.