LONDON:Jeshi la Uingereza kupunguzwa kutoka Irak | Habari za Ulimwengu | DW | 09.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON:Jeshi la Uingereza kupunguzwa kutoka Irak

Waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown amesema kwamba serikali yake inaazimia kupunguza idadi ya wanajeshi wake kutoka nchini Irak hadi kufikia askari 2,500.

Bwana Brown ameyasema hayo wakati alipolihutubia bunge, amesema hatua ya kwanza itaanza mara moja wakati ambapo Wairak wenyewe wameanza kutekeleza majukumu ya kulinda usalama.

Matamshi ya waziri mkuu wa Uingereza yamefuatia pendekezo lake la wiki moja iliyopita kwamba anatarajia kupunguza idadi ya askari 4,500 kufikia mwisho wa mwaka huu.

Waziri mkuu wa Uingereza Gordon Browm amesema kuwa maamuzi ya mwisho kuhusu kuwaondoa askari wa Uingereza kutoka nchini Irak yatapitishwa baada ya kushauriana na wakuu wa jeshi la Uingereza wa nchini Irak.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com