LONDON:Hali nchini Irak ni mbaya kuliko wakati wa Saddam Hussein | Habari za Ulimwengu | DW | 04.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON:Hali nchini Irak ni mbaya kuliko wakati wa Saddam Hussein

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan amesema,Irak tayari inajikuta katika hali ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.Katika mahojiano yake na BBC,Annan amesema,hali ya mambo nchini Irak ni mbaya zaidi kuliko ilivyokuwa hapo zamani huko Lebanon au katika nchi zingine.Si hilo tu,bali sasa watu wengi wanaishi katika hali mbaya zaidi kuliko ilivyokuwa chini ya utawala wa Saddam Hussein.Annan ambae muda wake unamalizika Desemba 31,kwa mara nyingine tena amependekeza kufanywe mkutano wa kimataifa kuhusu Irak.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com