LONDON : Watatu washtakiwa kwa miripuko ya London | Habari za Ulimwengu | DW | 06.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON : Watatu washtakiwa kwa miripuko ya London

Watuhumiwa watatu waliokamatwa nchini Uingereza mwezi uliopita wamefunguliwa mashtaka ya kuhusika na mashambulizi ya kujitolea muhanga maisha kwa kujiripuwa ya tarehe 7 mwezi wa Julai mwaka 2005 mjini London ambapo wasafiri 52 waliuwawa.

Msemaji wa shirika la upelelezi la Scotland Yard amesema wanaume hao watatu wamehusika katika kupeleleza na kupanga mashambulizi hayo ya mabomu.

Katika mashambulizi hayo washambuliaji wanne wa kujitolea muhanga maisha walijiripuwa kwenye treni za chini ya ardhi na kwenye basi moja.

Watu hao watatu watafikishwa mahkamani kwa mara ya kwanza hapo Jumamosi.

Polisi wanasema wanategemea kuwakamata watu zaidi kuhusiana na kesi hiyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com