1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Washukiwa wa ugaidi wahukumiwa Uingereza.

16 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBrP

Mahakama ya London imewahukumu watu saba kifungo cha kati ya miaka kumi na mitano na miaka ishirini na sita gerezani kwa kupanga njama ya kuwaua maelfu ya watu nchini Uingereza na Marekani.

Kiongozi mkuu wa njama hiyo, Dhiren Bharot, ambaye viongozi wa mashtaka wanasema ana uhusiano na kundi la al-Qaeda, yumo gerezani anakotumikia kifungo cha miaka thelathini.

Kwa mujibu wa mahakama hiyo, watu hao saba walishirikiana na Dhiren Barot kupanga njama ya kushambulia mji wa London kwa bomu lenye miale ya sumu, kuvuruga usafiri wa magari- moshi na pia kuteketeza maegesho ya chini kwa chini ya magari kwa mabomu yaliyotegwa kwenye magari ya kifahari.

Watu sita miongoni mwa washtakiwa hao walikuwa wamekiri mashtaka yao.

Mshukiwa wa saba alipatikana na hatia wakati kesi hiyo ilipokuwa ikiendeshwa.