1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Uingereza yazuia kwa hiyari usafirishaji wa mifugo

5 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBbt

Uingereza inajaribu kudhibiti mripuko wa ugonjwa wa miguu na midomo uliogunduliwa katika ngombe kwenye shamba moja,kusini mwa nchi hiyo.Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown amesema,anaelewa wasiwasi uliokuwepo hivi sasa.Akaongezea kuwa kila kiwezekanacho kinafanywa,ili kuweza kupata ushahidi wa kisayansi na kujua chanzo cha ugonjwa huo na hatimae kuutokomeza Uingereza.

Serikali ya Uingereza,imeamaua kwa hiyari kupiga marufuku usafirishaji wa mifugo na bidhaa za wanyama.Ugonjwa wa miguu na midomo,uliporipuka mwaka 2001,mifugo milioni 7 iliuliwa na uliathiri vibaya sana sekta za kilimo na utalii.