1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Uingereza kuiachia serikali ya Irak ulinzi wa mji wa Basra mwakani

23 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCqI

Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza, bibi Margaret Beckett, amesema huenda Uingereza ikawakabidhi viongozi wa Irak jukumu la ulinzi wa mji wa Basra, kusini mwa nchi kati ya mwezi wa Februari na Juni mwaka ujao. Kwa sasa kuna wanajeshi 7,000 kutoka Uingereza katika eneo la mji wa Basra.

Waziri Beckett, amesema maendeleo ambayo yamepatikana siku za hivi karibuni, yamemtia moyo kwamba serikali ya mpito inaweza kuchukuwa usukani wa kulinda usalama mnamo miezi ijayo.

Wakati hayo yakiarifiwa, idadi ya raia wa Irak waliouawa mnamo mwezi uliopita wa Oktoba imefikia kiwango cha juu kabisa kuwahi kufikiwa.

Ripoti ya Umoja wa mataifa inasema zaidi ya raia 3,700 waliuawa na hivyo kuzidi rikodi mbaya ya mauaji yaliyotokea mwezi Julai mwaka huu.