1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Uingereza itasaidia vikosi vya amani Darfur

16 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBPK

Waziri Mkuu wa Uingereza,Gordon Brown ameahidi kusaidia mipango ya ugavi na usafirishaji wa watu na zana,kwa vikosi vya amani vya kimataifa,ambavyo vinatazamiwa kupelekwa katika jimbo la mgogoro la Darfur,nchini Sudan. Amesema,serikali yake ipo tayari pia kutoa msaada wa kiuchumi ikiwa makubaliano ya kisiasa na kuweka chini silaha yatapatikana kati ya makundi yanayohasimiana nchini Sudan.

Wakati huo huo,Gordon Brown akaonya,hatua za kuiwekea vikwazo zaidi itachukuliwa dhidi ya Sudan ikiwa serikali ya Khartoum haitofanya mageuzi yanayohitajika.Brown,anaamini kuwa Marekani na serikali za Ulaya pia zitakuwa tayari kuunga mkono hatua hiyo.