LONDON : Sita washtakiwa kwa ugaidi | Habari za Ulimwengu | DW | 10.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON : Sita washtakiwa kwa ugaidi

Watu sita wamefunguliwa mashtaka kufuatia misako dhidi ya ugaidi nchini Uingereza wiki iliopita ambapo mmoja wao anakabiliwa na madai kuhusiana na njama ya kumteka nyara na kumuuwa askari wa Kiislam wa Uingereza.

Parviz Khan mwenye umri wa miaka 36 anashatakiwa pamoja na wenzake watano chini ya sheria ya kupiga vita ugaidi kufuatia kukamatwa kwa watu tisa katika misako ya alfajiri kwenye mji wa kati wa Uingereza wa Birmingham.Khan na watu wengine wanne wamefikishwa mahkamani mjini London hapo jana na wamerudishwa rumande.

Mtu wa sita anatazamiwa kufikishwa mahkamani leo hii wakati watu watu wengine watatu wameachiliwa huru bila ya kufunguliwa mashtaka.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com