LONDON : Sacramella hana sumu ya miale ya nuklea | Habari za Ulimwengu | DW | 02.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON : Sacramella hana sumu ya miale ya nuklea

Mtu aliekuwa na mawasiliano ya karibu na mpelelezi wa zamani wa Urusi Alexander Litvinenko ambaye amekufa baada ya kuonekana kuwa ametiwa sumu ya miale ya nuklea hakuna ishara inayoonyesha kwamba naye pia ameathiriwa na sumu hiyo ya miale ya nuklea.

Msemaji wa hospitali ya Chuo Kikuu ambapo Litvinenko pia alilazwa kabla ya kufa kwake amesema Mario Scaramella yuko katika hali nzuri na kwamba vipimo vimeonyesha kwamba hana sumu hiyo ya miale ya nuklea.

Awali ilielezwa kwamba Sacramella ambaye anajiita mtaalamu wa usalama wa kujitegemea alikuwa ameathirika na sumu hiyo na vyombo vya habari vya Uingereza viliripoti kwamba hali yake ilikuwa mbaya.

Mjane wa Litvinenko pia ameonyesha ishara ya kuwa na sumu hiyo ya miale ya nuklea.

Wakati huo huo gazeti la Uingereza la Guardian limesema kwamba limeambiwa kuwa dozi ya sumu hiyo ya miale ya nuklea iliotumika kumuuwa Litvinenko yumkini ikawa imegharimu mamilioni ya euro.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com