1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Mwito wa kuondosha vikosi vya Kingereza kutoka Irak

13 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD3P

Kamanda wa majeshi ya Uingereza wa ngazi ya juu ametoa mwito wa kuviondoa mapema vikosi vya Kingereza kutoka Irak.Jemadari Richard Dannatt amesema kuendelea kuwepo kwa vikosi vya Kingereza nchini Irak,kunasababisha hali ya usalama nchini humo kuwa mbaya zaidi.Katika mahojiano yake na gazeti la Kingereza la “Daily Mail”,Jemadari Dannatt amesema,harakati za Uingereza nchini Irak,zinaongeza vitisho katika sehemu zingine za ulimwengu dhidi ya nchi za magharibi.Ripoti zinasema kuwa ofisi ya waziri mkuu Tony Blair haikuwa na habari kuhusu matamshi ya jemadari Dananat na haikutoa maelezo yo yote.Uingereza ni mshirika mkuu wa Marekani nchini Irak na ina wanajeshi 7,000 nchini humo.Wanajeshi 119 wa Kingereza wameuawa nchini Irak,tangu vikosi vya muungano,chini ya uongozi wa Marekani kuivamia Irak mwaka 2003 na kumuondosha madarakani Saddam Hussein.