LONDON : Msako wa muuaji wa makahaba waendelea | Habari za Ulimwengu | DW | 14.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON : Msako wa muuaji wa makahaba waendelea

Nchini Uingereza msako mkubwa unaendelea kumtafuta mtuhumiwa wa vifo vya makahaba.

Polisi inatuhumu kwamba muaji anayeuwa watu mfululizo amewalenga makahaba.Maiti tano zimepatikana karibu na mji wa mashariki wa Uingereza wa Ipswich katika kipindi cha siku 10.

Wapelelezi wamezitambuwa maiti tatu za wanawake waliouwawa kuwa za makahaba na wamesema wanatuhumu maiti nyengine mbili kuwa pia zinaweza kuwa ni za makahaba kutoka Ipswich ambao huko nyuma iliripotiwa kuwa hawajulikani walipo.

Waziri Mkuu wa Uingereza Tony Blair amesema serikali yake inaunga mkono polisi kwa kila hali katika kumtia mikononi muuaji huyo alieihamanisha Uingereza nzima.

Jarida mashuhuri la Jumapili nchini Uingereza News of the World limetowa zawadi isiowahi kutolewa kabla ya paundi 250,000 sawa na euro 372,000 kwa kukamatwa kwa mtu huyo waliempachika jina la Mnyongaji wa Suffolk.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com