London. Malkia awaonya wanaotaka kutumia dini vibaya. | Habari za Ulimwengu | DW | 31.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

London. Malkia awaonya wanaotaka kutumia dini vibaya.

Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia amekutana na waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown leo kujadili masuala ya ugaidi, amani ya mashariki ya kati , pamoja na mkwamo kuhusu mpango wa kinuklia wa Iran kama sehemu ya ziara yake ambayo imeleta upinzani mkubwa.

Mfalme Abdullah ambaye pia ni waziri mkuu , ameishutumu Uingereza kwa kutofanya juhudi zaidi kupambana na ugaidi.

Akizungumza na malkia wa Uingereza mwanzoni mwa ziara yake jana , malkia amesema kuwa mataifa duniani yanapaswa kuwa pamoja ili kupambana na watu wanaotaka kutumia dini vibaya.

Brown ameieleza Saudi Arabia kuwa ni mshirika muhimu katika mashariki ya kati. Hii ni ziara ya kwanza kwa kiongozi huyo wa taifa la Kiislamu katika miongo miwili.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com