1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Homa ya ndege yagunduliwa nchini Uingereza.

4 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCV9

Maafisa wa afya nchini Uingereza wamethibitisha batamzinga zaidi ya elfu mbili wamekufa kwenye shamba moja mashariki mwa nchi hiyo, kutokana na homa ya ndege inayosababishwa na virusi vya H5N1.

Homa hiyo tayari imesababisha vifo vya watu zaidi ya mia moja na sitini kote duniani tangu miaka minne iliyopita.

Watu wengi waliofariki kutokana na homa hiyo wanatoka barani Eshia.

Shamba hilo linalopatikana katika eneo la Suffolk, ni mali ya kampuni kubwa ya ufugaji wa batamzinga barani Ulaya.

Polisi wamelizingira eneo hilo na bata mzinga laki moja na elfu sitini waliobaki wamepangwa kuuawa haraka iwezekanavyo.

Maafisa wa afya wamesema hali imedhibitiwa.