LONDON : Aidha Brown au Mugabe katika mkutano Ureno | Habari za Ulimwengu | DW | 21.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON : Aidha Brown au Mugabe katika mkutano Ureno

Waziri Mkuu wa Uingerea Gordon Brown amependekeza vikwazo vipya dhidi ya Zimbabwe hapo jana na ametishia kususia mkutano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika hapo mwezi wa Desemba iwapo Rais Robert Mugabe atahudhuria mkutano huo.

Serikali mjini Harare imesema Brown anapoteza muda wake kwa kuonya kwamba atasusia mkutano huo nchini Ureno na kusisitiza kwamba Rais Mugabe mwenye umri wa miaka 83 amealikwa na kwa hiyo atahudhuria mkutano huo na arais wa nchi jirani ya Zambia amesema atausia mkutano huo iwapo Mugabe atatolewa.

Waziri wa mambo ya nje wa Ureno Luis Amado baadae amesema angelipendelea Brown ahudhurie mkutano huo kuliko Mugabe lakini bado hakua mialiko iliyotolewa na kwamba atalishughukilia suala hilo katika siku chache zijazo.Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com