1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Loew afurahishwa na maendeleo ya timu ya taifa

Sekione Kitojo
3 Juni 2019

Joachim Loew afurahishwa na maendelea aliyopiga kuijenga upya timu ya taifa ya Ujerumani Die Mannschaft

https://p.dw.com/p/3JjEN
Fußball Nationalmannschaft Amsterdam Jogi Löw
Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim LoewPicha: picture-alliance/GES/M.I. Güngör

Kwa upande wa  timu  ya  taifa  ya  Ujerumani, kocha  Joachim Loew amesema  kufufuka  kwa  timu  ya  taifa  kumekuwa  hatua  nzuri sana , baada ya  kuondolewa  katika  hali  ya  kukatisha  tamaa  na kwa  fedhaha katika  fainali  za  kombe  la  dunia  mwaka  2018 nchini  Urusi.

Joachim Löw und Manuel Neuer
Kocha JoachimLoew (kulia) na mlinda mlango wa timu ya Ujerumani Manuel NeuerPicha: picture-alliance/dpa/J. Stratenschulte

Katika  mahojiano  na  gazeti  la  michezo  la Kicker, Loew  alikiri kwamba  hakuona mapungufu yaliyopo yataathiri utendaji  wa  timu yake baada  ya  miezi 12  iliyopita  kushuhudia awamu  ya  kufuzu iliyokuwa sahihi  kabisa pamoja  na  iúbingwa  wa  kombe  la shirikisho, Confederation. Baada ya  kombe  la  dunia alitarajia wachezaji kuamka  katika  ligi  ya  mataifa, lakini  baada  ya  kipigo cha  mabao 3-0 dhidi  ya  Uholanzi  mwezi  Oktoba  alitanabahi kwamba  "muda  sasa  umewadia  wa  mabadiliko".