Livni na Netanyahu kila mmoja adai kushinda uchaguzi Israel | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 11.02.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Livni na Netanyahu kila mmoja adai kushinda uchaguzi Israel

Mvutano wa nani mshindi katika uchaguzi mkuu wa Israel umejitokeza huku vyama viwili vya Likud na Kadima vikidai kushinda

Kiongozi wa chama cha Kadima Tzipi Livni

Kiongozi wa chama cha Kadima Tzipi Livni

Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Tzipi Livni na Waziri Mkuu wa zamani Benjamin Netanyahu kila mmoja ametangaza kuwa ameshinda katika uchaguzi huo mkuu wa hapo jana.


Wakati ambapo asilimia 91 ya kura zimekwishahesabiwa, vituo vya televisheni vya nchi hiyo vimesema kuwa chama cha Kadima cha Bi Livni kinaongoza kwa viti viwili dhidi ya kile cha Likud kinachoongozwa na Netanyahu.


Lakini Waziri huyo mkuu wa zamani wa Israel akiwahutubia wafuasi wa chama chake amesema kuwa ana hakika ataongoza serikali ijayo.


Kwa upande wake Bi Livni aliwaambia wafuasi wake kuwa chama chake cha Kadima kimeshinda na kumuomba Netanyahu kujiunga naye katika serikali ya umoja atakayoingoza.


Matokeo rasmi yanategemewa kutangazwa baadaye hii leo.

 • Tarehe 11.02.2009
 • Mwandishi Aboubakary Jumaa Liongo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GrGp
 • Tarehe 11.02.2009
 • Mwandishi Aboubakary Jumaa Liongo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GrGp
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com