1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Liverpool wawabwaga Arsenal

26 Agosti 2019

Katika Ligi Kuu ya England mechi kubwa mwishoni mwa wiki ilikuwa kati ya Liverpool na Arsenal ambapo Arsenal walinyamazishwa na hao makamu bingwa msimu uliopita kwa kushindiliwa mabao matatu kwa moja.

https://p.dw.com/p/3OVGA
UEFA Champions League Finale | Tottenham Hotspur v FC Liverpool Mo Salah
Picha: AFP/G. Bouys

Mo Salah ndiye aliyeng'ara katika mtanange huo kwani alipachika wavuni mabao mawili ya Liverpool na Joel Matip akafunga pia. Arsenal walipewa la kufutia jasho na kiungo wao Lucas Torreira.

Manchester United walikuwa nyumbani lakini walishangazwa na Crystal Palace kwa kufungwa magoli mawili kwa moja.

Marcus Rashford alikosa mkwaju wa penalti katika mechi hiyo na kama Paul Pogba katika mechi dhidi ya Wolves walipotoka sare ya bao moja, alishambuliwa kwa maneno ya kibaguzi katika mtandao wa kijamii wa Twitter, jambo lililolaaniwa na kocha Ole Gunnar Solksjaer.

"Siamini kabisa kama tunazungumzia suala hili mwaka wa 2019. Bila shaka Twitter ni mtandao wa kijamii ambao watu wanaweza kujificha kwa vitambulisho bandia. Nafikiri si jukumu langu kubadilisha lakini ni sharti tufanye kitu kuhusiana na suala hili," alisema Solksjaer.