Liverpool walazimishwa sare, United na City watabasamu | Michezo | DW | 27.01.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Liverpool walazimishwa sare, United na City watabasamu

Huko England mwishoni mwa wiki mechi zilizochezwa zilikuwa ni za FA Cup iliyokuwa katika raundi ya nne na Manchester City na Manchester United walivuna ushindi mkubwa ambapo City waliwalemea Fulham mabao manne kwa bila.

Wakati huo huo United waliambulia ushindi wa sita bila walipokuwa ugenini kucheza na Tranmere.

Liverpool walikuwa wanacheza na Shrewsbury Town na kocha Jurgen Klopp alifanya mabadiliko mengi katika kikosi chake na mechi hiyo ikaishia sare ya mabao mawili kwa mawili. Sasa Liverpool watalazimika kucheza mechi ya marudiano na Shrewsbury uwanjani Anfield ingawa Klopp amesema hata katika mechi hiyo ya marudiano hatokichezesha kikosi chake cha kwanza kwani wachezaji hao wanastahili kupumzika.

Usiku wa Jumatatu AFC Bournemouth watakuwa wanawakaribisha Arsenal katika mechi nyengine ya kinyang'anyiro hicho cha FA Cup.