1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LISBON: Mkataba mpya wa Umoja wa Ulaya wakubaliwa

19 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Eb

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanaokutana mjini Lisbon,Ureno wameukubali mkataba mpya wa mageuzi,baada ya kuondosha upingamizi wa Poland na Italia.Upingamizi huo ulizusha mivutano na kuchelewesha maafikiano.

Sasa,Italia imepewa kiti kimoja zaidi katika bunge jipya la Ulaya.Poland nayo,imeridhishwa na kura ya turufu itakayoweza kutumiwa kupinga maamuzi yatakayopitishwa kwa uwingi mdogo.Lakini kura hiyo baadae inaweza kuondoshwa kwa makubaliano ya viongozi wote wa umoja huo.

Mkataba uliokubaliwa unaweka msingi mpya wa Umoja wa Ulaya.Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel amesema,mkataba huo mpya wa mageuzi,unatazamiwa kutiwa saini Desemba 13 mjini Lisbon.