LISBON: Kadi Buluu kuvutia wataalamu wajuzi | Habari za Ulimwengu | DW | 13.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LISBON: Kadi Buluu kuvutia wataalamu wajuzi

Kamishna wa sheria wa Umoja wa Ulaya,Franco Frattini amesema mwezi ujao atazindua “Kadi Buluu ya Leba“ ya Umoja wa Ulaya.Alipozungumza mjini Lisbon nchini Ureno kwenye mkutano uliohusika na masuala ya uhamiaji,Frattini alisema,pendekezo hilo litawasilishwa kwa wanachama 27 wa Umoja wa Ulaya tarehe 23 Oktoba.

Azma ya mradi huo ni kuwavutia Ulaya,wataalamu wenye ujuzi ambao wanatafuta ajira.Kadi Buluu itawapa wafanyakazi wenye ujuzi mkubwa,haki mbali mbali kuhusu usalama wa kijamii na hali za kufanya kazi katika nchi za Umoja wa Ulaya.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com