1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LIMA: Peru yatangaza hali ya tahadhari

17 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBYQ

Serikali ya Peru imetangaza hali ya hatari na siku tatu za maombolezi rasmi ya kitaifa kufuatia tetemeko la ardhi lililowaua mamia ya watu nchini humo.

Timu ya waokoaji inajaribu kukabiliana na athari zilizosababishwa na mtetemeko huo. Mitetemeko mingine midogo imetokea katika mji mkuu wa Peru, Lima, huku maafisa katika eneo wakitathimini uharibifu uliosababishwa na tetemeko hilo la ardhi la kiwango cha 7.9 kwenye kipimo cha Richter.

Watu takriban 500 waliuwawa kwenye mtetemeko huo na mashirika ya misaada yanaripoti kuwa zaidi ya watu wengine 1,000 wamejeruhiwa.

Maelfu ya watu wamepoteza makaazi yao baada ya nyumba zao kuanguka.

Kitovu cha tetemeko hilo kiko katika bahari ya Pacific, yapata kilomita 148 kusini magharibi mwa mji wa Lima.