1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ligi ya Ulaya: Bayern kukutana tena na Arsenal

28 Agosti 2015

Droo ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya – UEFA Champions League imezikutanisha timu tatu za Ujerumani na wapinzani wa Uingereza, wakati Bayer Leverkusen ikipangwa na mabingwa watetezi Barcelona

https://p.dw.com/p/1GNZ6
Arsenal FC vs Bayern Munich
Picha: Reuters

Mabingwa wa Ujerumani Bayern watashuka dimbani na Arsenal kwa mara ya tatu katika misimu minne, lakini watacheza dhidi ya Gunners katika hatua ya makundi na sio awamu ya muondowano kama ilivyokuwa katika misimu miwili iliyopita. Davod Miles ni Katibu wa Arsenal "Droo ilianza katika njia ya kushangaza tulipopewa Bayern Munich na ni wazi kuwa ilivyoendelea ilituondolea shinikizo kiasi hasa kuhusu ugumu uliopo. Lakini huu ni msimu wetu wa 18 mfululizo katika hatua y amakundi ya Champions League, kitu ambacho nadhani ni ushuhuda mzuri kwa Arsene Wenger na kile alichokifanyia klabu hii. Hivyo tunajiandaa kwa mpambano".

Mbali na Arsenal, vijana wa Pep Guardiola Bayern watahitajika pia kuwazidi nguvu Olympiakos ya Ugiriki na Dynamo Zagreb ya Croatia ili kuendeleza matumaini yao ya kushinda ubingwa wa Ulaya.

Bundesliga Fussballspiel FC Koeln v VfL Wolfsburg 22.08.2015
Wolfsburg watalenga kufanya vyema katika jukwaa la Ulaya bila ya mchezaji wao Kevin de BruynePicha: Getty Images/AFP/P. Stollar

Washindi wa kombe la shirikisho la Ujerumani msimu uliopita Wolfsburg watapambana na Manchester United ya Louis van Gaal, pamoja na PSV Eindhoven na CSKA Moscow. Wolfsburg walishindwa na United katika hatua ya makundi katika msimu wa 2009 - 2010.

Borussia Moenchengladbach itahataji kuongeza kasi yao msimu huu, itakapopambana na na Juventus waliofika fainali msimu uliopita, Manchester City na washindi wa Europa Legaue Sevilla. Giuseppi Marotta ni mkurugenzi wa michezo wa Juve "droo inaweza kuhamasisha sana kwa mfano kundi letu lina timu za kiwango sawa. Lakini sisi ni Juventus hivyo tunafahamu tunastahili kushiriki ili kufuzu. Hivyo tutapambana na matumaini makubwa.

Bayer Leverkusen, watachuana na AS Roma. Lakini kibarua kikubwa kwa vijana hao wa kocha Roger Schmidt ni dhidi ya mabingwa wa mwaka jana Barcelona.

Kwingineko, Paris Saint-Germain wamepangwa dhidi ya mabingwa wa Sweden Malmo pamoja na miamba ya Uhispania Real Madrid na mabinhwa wa Ukraine Shakhtar Donetsk. Mabingwa wa England Chelsea watakutana na Porto ambako kocha Jose Mourinho alishinda Champions League na klabu hiyo kitu ambacho balozi wa Chelsea Carlo Cudicini anasema ni muhimu "ni kundi gumu, kwa sababu tofauti. Kitu kiguri ni kuwa kocha wetu anaifahamu Porto vyema, lakini kwa vilabu vingine viwili ni mbali kusafiri kuchuana na Dynamo Kiev, katikati ya wiki huwa sio rahisi. Na macabi ni mabingwa wa Israel na kocha wao ni mchezaji wa zamani wa Chelsea hivyo ni kundi zuri".

Duru ya kwanza ya michuano hiyo itachezwa Septemba 15 na 16.

Droo kamili:

Group A: Paris SG, Real Madrid, Shakhtar Donestk, Malmo

Group B: PSV, Manchester United, CSKA Moscow, Wolfsburg

Group C: Benfica, Atletico Madrid, Galatasaray, Astana

Group D: Juventus, Manchester City, Sevilla, Borussia Mönchengladbach Group E: Barcelona, Bayer Leverkusen, Roma, BATE Borisov

Group F: Bayern Munich, Arsenal, Olympiacos, Dinamo Zagreb

Group G: Chelsea, Porto, Dynamo Kyiv, Maccabi Tel-Aviv

Group H: Zenit, Valencia, Lyon, Gent

Mwandishi. Bruce Amani/DW/AFP/DPA/AP/reuters
Mhariri: Mohamed Khelef