Ligi ya Mabingwa Ulaya yaendelea kutimua vumbi | Michezo | DW | 24.02.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Ligi ya Mabingwa Ulaya yaendelea kutimua vumbi

Manchester City wamepigwa marufuku kushiriki mashindano ya Champions League kwa misimu miwili ijayo lakini kwa sasa wanalenga kutinga robo fainali ya mashindano ya msimu huu wakati watashuka dimbani dhidi ya Real Madrid

Manchester City wamepigwa marufuku kushiriki mashindano ya Champions League kwa misimu miwili ijayo lakini kwa sasa wanalenga kutinga robo fainali ya mashindano ya msimu huu wakati watashuka dimbani siku ya Jumatano na Real Madrid katika hatua ya 16 za mwisho.

Itakuwa mechi ya kwanza ya City tangu walipopigwa marufuku na UEFA kwa kukiuka sheria za usawa wa kifedha lakini wanasema watakata rufaa katika mahakama ya Usuluhishi michezoni.

Barca kwa upande wao watakwenda Napoli kesho Jumanne, zikiwa ni mechi za kwanza kabisa kwa makocha wa timu hizo, na katika siku hiyo, Bayern watawatembelea Chelsea katika mtanange wa marudio wa fainali ya 2012 ambayo Chelsea walishinda kwa penalty mjini Munich. Mechi nyingine ya Jumatano ni Juventus yake Cristiano Ronaldo dhidi ya Wafaransa Olympique Lyon.