1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hukumu ya kifungo cha maisha dhidi ya Roger Lumbala?

13 Desemba 2025

Waendesha mashtaka nchini Ufaransa wametaka adhabu ya kifungo cha maisha jela kwa kiongozi wa zamani wa waasi Roger Lumbala anayetuhumiwa kuwa mmoja wa waratibu wa ukatili katika Vita vya Pili vya Kongo.

https://p.dw.com/p/55HfA
Roger Lumbala
Kiongozi wa waasi wa M23 Roger Lumbala (kushoto) asaini hati kabla ya kikao na waandishi wa habari mnamo Februari 6, 2013Picha: Isaac Kasamani/AFP/Getty Images

Lumbala, mwenye umri wa miaka 67, ameshtakiwa mjini Paris kwa kuhusika na uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa mzozo huo wa 1998-2003 mashtaka ambayo amekanusha.

Lumbala, ambaye alikamatwa nchini Ufaransa Desemba 2020, alikataa kuhudhuria kikao cha ufunguzi cha kesi hiyo dhidi yake, na kusema mahakama hiyo haina uhalali.

Lumbala ambaye alihudumu kwa muda mfupi kama waziri wa biashara wa kongo kisha akagombea urais mwaka 2006, anasisitiza kuwa alikuwa mwanasiasa asiye na jeshi wala watu wa kujitolea chini ya udhibiti wake.

Lakini mmoja wa waendesha mashtaka Nicolas Péron, aliliambia jopo la majaji kwamba Lumbala anakosa kuhudhuria kesi hiyo kwa sababu "anakabiliwa na tatizo ambalo hajawahi kufikiria angeweza kukumbana nalo, kwamba sasa anakabiliwa na haki".

Hukumu dhidi yake inatarajiwa kutolewa siku ya Jumatatu.