1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Libya imekwama katika mgogoro, aonya mjumbe wa UN

Bruce Amani
16 Julai 2021

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, Jan Kubis ameonya kuhusu mkwamo wa kisiasa, usalama na mipango ya bajeti kwa nchi hiyo, ambayo inapaswa kuandaa uchaguzi mkuu Desemba 24 lakini umbao unaonekana kutiliwa mashaka.

https://p.dw.com/p/3wZIc
Jan Kubis (C) Sonderbeauftragter des UN-Generalsekretärs für den Irak
Picha: picture-alliance/Photoshot

Akizungumza katika mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu Libya wa ngazi ya mawaziri, Kubis ameelezea wasiwasi kuhusu madhara ya mkwamo huo kwa mchakato wa uchaguzi na kisiasa.

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa kuna zaidi ya mamluki 20,000, wakiwemo Warusi, Wasyria, Wachad na Wasudan na wanajeshi wa kigeni, wengi wao Waturuki, wanaopigana nchini Libya.

Mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa pia ameashiria kuwa bajeti haiwezi kuidhinishwa wiki hii na kuwa mishahara ya wahudumu kwa upande wa upinzani haijalipwa.

Mkutano huo ulihudhuriwa na Waziri Mkuu wa Libya Abdelhamid Dbeibah, Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian, ambaye nchi yake inashikilia urais wa Baraza la Usalama kwa mwezi Julai, wamesisitiza kuwa mafanikio yanawezakana Libya.