1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lewandowski ni moto wa kuotea mbali

7 Oktoba 2019

Mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski anaendelea kuweka rekodi moja baada ya nyengine.

https://p.dw.com/p/3QqJL
Tottenham Hotspur - FC Bayern München
Picha: picture-alliance/dpa/M. Balk

Baada ya kufunga goli moja la Bayern kwenye mechi yao iliyopita raia huyo wa Poland alifikisha idadi ya magoli yake katika Bundesliga kufikia 213 na kujiunga na Manfred Burgsmueller katika nafasi ya nne ya orodha ya wafungaji bora zaidi wa Ligi Kuu ya Ujerumani.

Lewandowski pia amefunga katika kila moja ya mechi kumi zilizopita katika mashindano yote na kwa sasa ana jumla ya magoli 15 msimu huu.