Lewandowski apigwa na kiripuzi | Michezo | DW | 12.11.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Lewandowski apigwa na kiripuzi

Mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski aliangukiwa na fashifashi iliyorushwa kutoka jukwaa la watazamaji katika pambano lililokuwa na hamasa nyingi kati ya Poland na Romania.

Fußball WM-Qualifikation Rumänien gegen Polen (picture alliance/dpa/R. Ghement)

Mchezaji Robert Lewandowski akiwa amelala chini baada ya kupigwa na fashifashi

Mshambuliaji  wa  Poland  Robert  Lewandowski  aliangukiwa  na fashifashi  iliyorushwa  kutoka  jukwaa  la   watazamaji   katika pambano  lililokuwa  na  hamasa  nyingi  jana  Ijumaa ,  lakini hatimaye  ndie  aliyetoka  uwanjani  akitabasamu , baada  ya kufunga  mabao mawili   katika  ushindi  wa  mabao 3-0  dhidi  ya Romania.

Mashabiki  wa  Romania  walirusha  fashifashi  dhidi  ya  nyota  huyo wa  Bayern  Munich  katika  dakika  ya  53. Alihitaji  matibabu  kidogo wakati  refa  Damir Skomina  aliwakusanya  wachezaji  wa  pande zote  katikati  ya  uwanja.

Baada  ya  mchezo  huo  kusitishwa  kwa  muda , Lewandowski aliweza  kufunga  mabao mawili  baada  ya  dakika  84  pamoja  na penalti  ya  dakika  za  mwisho.

Kwa  upande  wa  watazamaji ,  mashabiki  kutoka  kila  upande walirushiana   fashifashi. Baadhi zilizorushwa  na  mashabiki  wa nyumbani  ziliangukia  uwanjani , na  kusababisha  kucheleweshwa mchezo  huo  kuanza  kabla  ya  mapumziko. Mashabiki 12  wa poland  walikamatwa   kabla  ya  mchezo  huo  baada  ya  kuigana katika  baa  katikati  ya  mji  na  mapambano  na  polisi  nje  ya uwanja.

Fußball WM-Qualifikationsspiel Polen vs. Dänemark in Warschau (Reuters/Agencja K. Atys)

Robert Lewandowski mshambuliaji wa Poland

Nahodha  wa  Mexico Rafael Marquez  alifunga  bao  ushindi  katika dakika  ya  89  wakati  Mexico  ilipoishangaza  Marekani  kwa ushindi  wa  mabao 2-1  katika  pambano  la  kusisimua  la  kufuzu kucheza  katika   fainali  za  kombe  la  dunia  kati  ya   timu  hizo mbili  mahasimu  wakubwa  jana  Ijumaa.

Marquez , mwenye  umri  wa  miaka  37, alifunga  kwa  kichwa  mpira wa  kona  uliopigwa  na  Miguel Layun  katika  dakika  za  mwisho na ambapo  Bobby Wood  alisawazisha  hapo  kabla  bao  la  Mexico lililofungwa  na  Layun  katika  dakika  ya  20 ya  mchezo.

Matokeo  mengine  katika  michezo  ya  kanda  ya  shirikisho  la CONCACAF  ni  Honduras ilikandikwa  bao 1-0  na  Panama , Trinidad  na  Tobago  ilisalimu  amri  mbele  ya  Costa  Rica  kwa kufungwa  mabao 2-0.

Mwandishi:  Sekione  Kitojo / afpe / rtre

Mhariri: Sylvia  Mwehozi