Lewandowski ahisi kusalitiwa na Dortmund | Michezo | DW | 02.08.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Lewandowski ahisi kusalitiwa na Dortmund

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Robert Lewandowski angali na hasira moyoni kutokana na hatua ya klabu yake kukataa kumruhusu ajiunge na mabingwa wa mataji matatu msimu uliopita Bayern Munich

epa03682984 Borussia Dortmund's Polish striker Robert Lewandowski reacts the UEFA Champions League semi final second leg match between Real Madrid and Borussia Dortmund at Santiago Bernabeu stadium in Madrid, central Spain, 30 April 2013. EPA/JUANJO MARTIN +++(c) dpa - Bildfunk+++

UEFA Champions League Halbfinal-Rückspiel Real Madrid - Borussia Dortmund

Lewandowski anasema hawezi kuficha ukweli kwamba anahisi alisalitiwa…kwa sababu maafisa wa klabu yake walimwambia kitu kimoja, na kitu hicho kikabadilika kabisa kinyume na jinsi walivyokubaliana.

Lewandoswki amesema Dortmund walivunja ahadi yao wakati walipokataa kumruhusu aondoke hadi mkataba wake utakapokamilika mwaka wa 2014 na kwamba nyongeza kubwa ya mshahara aliyoahidiwa kupewa katika msimu huu unaoanza bado haijaanza kutekelezwa.

Emre Can ni mmoja wa wachezaji chipukizi wenye vipaji katika soka la Ujerumani

Emre Can ni mmoja wa wachezaji chipukizi wenye vipaji katika soka la Ujerumani

Nyota huyo wa Poland hata hivyo ameahidi kufanya kila awezalo kuhakikisha kuwa Dortmund wanashinda mataji zaidi msimu huu, ijapokuwa anasema hajui kama hali ya sasa itaathiri mchezo wake. Kocha wa BVB Jurgen Klopp amesema kwamba klabu hiyo itafanya mkutano na Lewandowski ili kulitatua suala hilo kabla ya kuanza msimu mpya.

Emre Can ahamia Leverkusen kutoka Bayern

Kiungo wa timu ya taifa ya Ujerumani ya wachezaji walio na umri wa chini ya miaka 21 Emre Can amehama klabu ya Bayern Munich na kujiunga na klabu ya Bayer Leverkusen kwa kusaini mkataba wa miaka minne.

Huku Bayern ikiwa na wachezaji kumi viungo wa kimataifa, Can mwenye umri wa miaka 19 hakuhakikishiwa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza chini ya kocha mpya wa Bayern Pep Guardiola na hivyo anajiunga na Leverkusen ambao walifuzu moja kwa moja katika Ligi ya Mabingwa Ulaya. Bayern wana chaguo la kumnunua tena atakapokamilisha mkataba wake katika klabu ya Leverkusen.

Mwandishi: Bruce Amani/DPA/AFP/reuters

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman