Leverkusen mguu mmoja katika Champions League | Michezo | DW | 20.08.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Leverkusen mguu mmoja katika Champions League

Bayer Leverkusen wameizaba FC Copenhagen magoli matatu kwa mawili mjini Denmark, na kujiweka katika nafasi nzuri kabla ya mchuano wa marudiano wa kufuzu katika awamu ya makundi ya Champions League.

Magoli yote atano yalipatikana katika kipindi cha kwanza. Leverkusen walidhihirisha kile ambacho wachambuzi wengi wa kandanda walitabiri kuwa vijana hao wa kocha mpya Roger Schimdt watakuwa na mfumo wa kandanda ya kushambulia.

Stefan Kiessling, baada ya kufunga magoli matano katika mchuano wa Kombe la Shirikisho la Ujerumani – DFB mwishoni mwa wiki, alifungua ukurasa wa magoli baada ya dakika tano za mchezo kuanza baada ya kuandaliwa pasi safi na mchezaji mpya Hakan Calhanoglu.

Kisha dakika chache baadaye, Leverkusen wakadorora katika safu ya ulinzi na kuwaruhusu wenyeji Copenhagen kufunga bao la kusawazisha kupitia mchezaji Mathias Jorgensen aliyebusu wavu kwa kichwa. Kisha muda mfupi baadaye Daniel Amartey akaongeza la pili na kuwaweka wenyeji kifua mbele.

Champions League Qualifikation Bayer Leverkusen - FC Copenhagen

Heung - Min Son alifunga la tatu na kuipa Leverkusen ushindi dhidi ya Copenhagen

Wakati ikikaribia mwisho wa kipindi cha kwanza, Leverkusena wakapata bao safi kupitia mchezaji Karim Bellarabi na kufanya mambo kuwa mawili kwa mawili. Kisha kabla ya kipyenga cha kumalizika kipindi cha kwanza kupulizwa, Son HEUNG-min akafunga bao safi na kwuapa Leverkusen ushindi wa magoli matatu kwa mawili.

Arsenal wakabwa na Besiktas

Arsenal walitoka sare ya sifuri kwa sifuri ugenini dhidi ya Besiktas ya Uturukin katika mechi ambayo kiungo wa Arsenal Aaron Ramsey alionyeshwa kadi nyekundu zikiwa zimesalia dakika kumi mchezo kukamilika.

Katika mechi ya marudiano uwanjani Emirates, kocha Arsene Wenger anatarajiwa kuwachagua wachezaji wa Ujerumani Mesut Özil, Per Mertesacker na Lukas Podolski baada ya kurejea kutoka mapumzikoni.

Nchini Austria, magoli kutoka kwa Franz Schiemer na Jonatan Soriano yalionekana kuwapa Salzburg ushindi muhimu kabla ya mkondo wa pili hadi pale Emil Forsberg alipoifungia Malmo goli la kuwapa matumaini katika dakika ya tisini.

Kwingineko, goli la ugenini lake Iker Muniain huenda pia likasaidia sana Athletic Bilbao hata ingawa Gonzalo Higuain alihakikisha kuwa Napoli ilitoka sare ya goli moja kwa moja nyumbani. Nchini Romania, Alexandru Chipciu, ambaye tayari alikosa penalty, alifunga goli pekee lililoipa ushindi Steaua Bucharesti dhidi ya Ludogorets ya Bulgaria.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP

Mhariri: Yusuf Saumu