1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lehmann azusha hasira-Asafiri hadi mazoezini kwa helikopta

19 Septemba 2008
https://p.dw.com/p/FLT1
Jens LehmannPicha: picture-alliance/ dpa

Mlinda lango wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani na Arsenal ya Uingereza Jens Lehman ambaye sasa anaichezea kilabu ya ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga Stuttgart, amekosolewa vikali na Meya wa mji wa Berg kusini mwa Ujerumani. Tukio hilo limesababishwa na kitendo cha Lehmann kusafiri hadi mazoezini katika uwanja wa kilabu yake ya Stuttgart kwa helikopta. Picha za mlinda mlango huo zilitokeza jana Ijumaa magazetini akitoka kwenye helikopta iliomrusha kutoka nyumbani kwake masafa ya kilomita 250 kwa malipo ya euro 1.000. Watu kadhaa katika mji huo wa wakaazi 8,200 wameungana na Meya wao kulalamika vikali. Meya Rupert Mann alisema anatumai Lehman hatofanya hivyo tena na kama atarudia basi atakwenda binafsi kuzungumza . Lehmann alihama kutoka Arsenal ya England baada ya mkataba wake kumalizika na kujiunga na mabingwa wa 2007 Stuttgart akirudi katika ligi kuu bundesliga, kwa mkataba wa mwaka mmoja.