LAS PALMAS : Mteka nyara ndege mbaroni | Habari za Ulimwengu | DW | 16.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LAS PALMAS : Mteka nyara ndege mbaroni

Polisi katika mji wa Las Palmas kwenye visiwa vya Canary vya Uhispania imesema imemtia nguvuni mtu mwenye silaha ambaye aliiteka nyara ndege ya abiria ya shirika la ndege la Mauritania Air Mauritania na kujaribu kuwalazimisha wafanyakazi wake wampeleke Ufaransa.

Kulikuwa na abiria 71 ndani ya ndege hiyo.

Polisi iliivamia ndege hiyo wakati ilipowasili Las Palmas kwa ajili ya kujaza mafuta.Abiria kadhaa walijeruhiwa wakati mtekaji nyara huyo alipokuwa akidhibitiwa.

Ndege hiyo aina ya Boeing 737 ililazimishwa kubadili safari wakati ikiwa safarini kutoka mji mkuu wa Mauritania Nouakchott kuelekea Nouadhibou mji mkuu wa pili kwa ukubwa nchini humo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com