1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LAGOS: Wafanyakazi wawili wauwawa na wengine watano kutekwa nyara

4 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD6Q

Wanamgambo waliyavamia makaazi ya wafanyakazi wa kigeni wa kampuni ya mafuta mjini Eket, kusini mwa eneo la Delta nchini Nigeria hapo jana na kuwaua walinzi wawili.

Habari zilizotolewa na kampuni ya mafuta ya ExxoMobil zinasema wafanyakazi watano walitekwa nyara katika uvamizi huo karibu na kiwanda cha kampuni hiyo.

Miongoni mwao ni raia watatu wa Uingereza na wawili wa Malaysia. Inaaminiwa walinzi wawili waliouwawa ni raia wa Nigeria. Msemaji wa kampuni ya ExxoMobil amesema hana habari zozote kuhusu kisa hicho.

Wakati huo huo, maofisa wa usalama wa Nigeria wanasema bado wanawatafuta wafanyakazi 16 wa kampuni ya Royal Dutch Shell ambao hawajulikani waliko tangu wanamgambo walipoushambulia msafara wao juzi Jumatatu. Wafanyakazi tisa wa kampuni ya Shell tayari wameachiliwa huru.

Muungano wa makundi ya wanamgambo umesema umefanya uvamizi huo na unataka kiongozi wake mmoja, Mujahid Dokubo-Asari, anayekabiliwa na kesi ya uhaini, aachiliwe huru.