LAGOS: Mgomo umeahirishwa baada ya maafikiano | Habari za Ulimwengu | DW | 26.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LAGOS: Mgomo umeahirishwa baada ya maafikiano

Vyama vya wafanyakazi katika sekta ya mafuta, nchini Nigeria,vimeahirisha mgomo wa siku mbili. Hatua hiyo imechukuliwa,baada ya serikali kukubali kutoa nyongeza ya mshahara na marupurupu.Mgomo huo ulihatarisha usafirishaji wa mafuta kutoka Nigeria,nchi iliyo mzalishaji mkuu wa nane wa mafuta duniani.Serikali imekubali kuongeza kwa asilimia 15,mishahara ya wafanyakazi wa kampuni la mafuta la Nigeria.Wakati huo huo nchini humo ambako kuna uhaba wa mafuta,tatizo hilo limezidi kuwa baya,ikiwa ni siku chache tu kabla ya serikali mpya kushika madaraka nchini. Rais mteule Umaru Yar ‘Adua anatarajiwa kumrithi Olusegun Obasanjo katika sherehe itakayofanywa siku ya Jumanne katika mji mkuu Abuja.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com