LAGA:.Jose Ramos-Horta kugombea kiti cha rais Timor Mashariki | Habari za Ulimwengu | DW | 26.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LAGA:.Jose Ramos-Horta kugombea kiti cha rais Timor Mashariki

Mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel na Waziri mkuu wa Timor Mashariki Jose Ramos-Horta ametangaza rasmi kwamba atajibwaga katika kinyang’anyiro cha kuwania kiti cha rais kwenye uchaguzi utakaofanyika mwezi Aprili.

Waziri mkuu Horta ameahidi kusaidia kurejesha amani na utulivu katika nchi hiyo iliyokumbwa na mizozo.

Timor Mashariki inakabiliwa na mzozo mkubwa kabisa tangu kujitenga na Indonesia mwaka 1999 na kujipatia uhuru wake mwaka 2002.

Tangu kuibuka mzozo wa kisiasa nchini humo jeshi la kulinda amani linaloongozwa na Australia limewekwa nchini humo kujaribu kutuliza hali ya mambo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com