Kwa nini dunia haitabadilika kwa ushindi wa Trump
10 Novemba 2016Uchaguzi ni Uchaguzi
Kutoka uchochezi wa hisia hadi uhalisia wa mambo. Wakati wa kampeini wagombea hutumia mbinu zote hata kama ni kupakana matope ili mradi tu waibuke na ushindi. Lakini baada ya ushindi ni wakati wa kuridhiana na kuleta taifa pamoja. Donald Trump alijaribu hilo katika hotuba yake ya kwanza. Hilo linatokana na kauli mbiu kuwa mtu habadili ofisi lakini wadhifa anaoshikilia unambadili. Aliyekuwa waziri wa kigeni wa Ujerumani Joscka Fischer tayari anaweza kuthibitisha haya. Trump ni mfanyibishara na atabadilika haraka kuweza kuona uhalisia ya mambo.
Ugunduzi wa uhusiano uliokuwa umepotea
Trump ni kiongozi wa tabaka la kati nchini Marekani. Tabaka ambalo limeathirika kijamii na kiuchumi katika kipindi cha miaka kadhaa iliyopita. Utawala uliko madarakani haukutilia maanani tabaka hilo la watu kwa miaka mingi. Kuvunjika moyo na kuhisi kuupuzwa kwa tabaka hilo katika taifa hilo lilofahamika kutokana na viwanda vyake ulimfanya Trump kupata kura nyingi ili kuwa mwakilishi wao na kuhakikisha anarejesha nafasi zaidi za kazi .
Uwekezaji wa ndani
Hakuna sera nzuri au sera mbaya muhimu ni inavyotekelezwa kuimarisha uchumi. Kauli mbiu ya Trump ya matumaini na mabadiliko imeleta mwanko mpya katika utawala wa Marekani.Inalenga kubadili sera za taifa, kuboresha miundo ya msingi kwa mfano mashule badala ya serikali kujitosa katika vita kama za Syria na Iraq. Sera za kiuchumi za Trump ndizo zitaamua mafanikio yake.
Mwanzo mpya kwa Marekani.
Marekani chini ya Rais Donald Trump ina nafasi nzuri ya kubadili mambo.Idadi kubwa ya waliompigia kura Trump inatumai hilo.Baadhi ya wachambuzi ambao wanamdhamini ushindi ambao haukutazamiwa wa bilionea huyo wanasema ushindi huo ni kama kilio cha uhuru. Mpasuko mkubwa wa miaka mingi nchini Marekani ambao unaonekana umeimarishwa na Ushindi wa Trump,unatoa nafasi nzuri ya kuyabadili maisha ya Wamarekani sio tu walio Manhattan hadi San Francisco lakini pia wananchi wa kawaida walio kusini na kati magharibi.Trump lazima atekeleze ahadi zake
Mwandishi:Jane Nyingi/Listicle-Wagener, Volker
Mhariri: Iddi Ssessanga