Kuzorota kwa hali ya usalama Uganda nani wa kulaumiwa?
10 Septemba 2018Museveni amesema kwamba serikali yake inaendelea kuimarisha usalama lakini inatatizwa na makundi ya watu wasioitakia mema Uganda mema yakiwemo mashirika yasio ya kiserikali, vyombo vya habari na wengine ambao wanawachochea wananchi kujenga hisia potofu dhidi ya utawala wake..
Akihutubia taifa usiku wa wa kumkia Jumatatu , rais Museveni amevilaumu pia vyombo vya habari kwa kusambaza kile alichokiita habari potofu kuhusu Uganda. Rais Museveni hata hivyo amekiri kuwa hali ya usalama inazidi kuzorota na atachukua hatua ya kuwarudisha askari wa mgambo.
Kwa upande mwengine raia wengi wamelezea kutoridhishwa kwao na mikakati yake kwani amekuwa akisema yaleyale wakati mauaji ya kikatili yanapotokea, kama vile ilivyokuwa mwishoni mwa juma lililopita wakati afisa wa polisi maarufu Muhamad Kirumira alipopigwa risasi na kuuwawa nje ya nyumbani kwake Jumamosi jioni.
Mwishoni mwa wiki iliopita, Kulizuka mchanganyiko wa maoni, hofu na hasira miongoni mwa raia kufuatia mauaji ya afisa maarufu wa polisi Muhamad Kirumira kukiwa na madai huenda polisi ilikuwa baada ya marehemu kueleza kwamba maafisa wenzake walishirikiana na magenge ya wahalifu.
Siku ya Jumapili rais Museveni alitangaza hatua kadhaa za kupambana na kile amnbacho kwa wengi wanakiona kuwa ni kuzorota kwa hali ya usalama. Ameagiza kuandikishwa kwa walinzi wa vijiji 24,000 ili kuisaidia polisi kupambana na uhalifu.
Katika hotuba yake kwa taifa, Museveni alisisitiza kuwa kamwe hatoruhusu watu ambao hawajui jinsi Uganda ilivyopata amani , kuivuruga amani hiyo .
Mwandishi: Lubega Emmanuel
Mhariri. Mohammed Abdul-Rahman