1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kuyaokoa mazungumzo ya amani Mashariki ya Kati

2 Oktoba 2010

Jumuiya ya Kimataifa inaendeleza harakati za kuyanusuru mazungumzo kati ya Israel na Palestina.

https://p.dw.com/p/PSe8
Mkuu wa sera za nje za Umoja wa Ulaya, Catherine Ashton.Picha: picture alliance / dpa

JERUSALEM

Mkuu wa sera za nje  wa  Umoja  wa Ulaya, Cathereine Ashton amemaliza ziara yake ya siku moja  nchini  Israel na katika maeneo ya  mamlaka  ya Palestina, huku akizitaka pande zote mbili ziendelee na mazungumzo ya amani.Akizungumza na waandishi  habari mjini Jerusalem, Ashton alisema mazungumzo yake na viongozi wa Israel pamoja na Wapalestina yalikuwa mazuri na yakutia moyo. Ashton alikuweko Jerusalem na Ramallah kujaribu kuyaokoa mazungumzo ya ana kwa ana kati ya pande hizo mbili yaliyoanza wiki nne zilizopita. Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas alisema mazungumzo hayo hayawezi kuendelea iwapo Israel itaendelea na ujenzi wa makaazi ya walowezi katika Ukingo wa Magharibi, eneo ambalo Wapalestina wana matumaini yatakuwa  sehemu  ya  taifa lao huru. Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesisitiza  nia ya kuendeleza mazungumzo hayo, lakini amekataa kusalim amri kwa shinikizo la Jumuiya ya Kimataifa kurefusha muda wa kusitisha ujenzi wa makaazi hayo ya Wayahudi uliomalizika wiki iliopita.