Kutekwa Goma na matumaini mema kwa Afrika | Magazetini | DW | 23.11.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Kutekwa Goma na matumaini mema kwa Afrika

Hali huko Goma ,kishindo kinachoikaba serikali ya Côte d'Ivoire na matumaini mema yanayowekewa bara la Afrika ni ada zilizoshughulikiwa na wahariri wa magazeti ya Ujerumani wiki hii.

Watu wanakimbia,M23 walipoingia Goma

Watu wanakimbia,M23 walipoingia Goma

Tuanzie lakini mashariki ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo.Hakuna hata moja ya magazeti mashuhuri ya Ujerumani ambalo halijazungumzia kisa cha waasi wa M23,kuuteka mji wa Goma,katika eneo tajiri la maadini mashariki ya jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo ."Waasi wa M23 watangaza azma ya kumpindua Kabila" ndio kichwa cha maneno cha uchambuzi wa Frankfurter Allgemeine.Siku mojaa baada ya kuuteka mji mkubwa wa Goma waasi wamelezea azma ya kusonga mbele.Frankfurter Allgemeine limenukuu msemaji wa waasi akisema"wataingia pia Bukavu,Kisangani na kufika hadi Kinshasa ikiwa rais Kabila hatong'atuka ."Waasi wamewataka watumishi wote wa idara za utawala warejee kazini.Hali imerejea kuwa ya kawaida na maduka yameshaanza kufunguliwa.Hata hivyo kuna ukosefu wa maji katika mji huo linaandika gazeti la Frankfurter linalozungumzia pia jinsi wananchi wanavyochukizwa na uongozi wa rais Kabila anaetuhumiwa kulipuuza jeshi kwasababu ya hofu lisije likampinduwa.Hata upande wa upinzani unamlaumu Kabila kuwa chanzo cha hali namna ilivyo katika eneo la mashariki.Frankfurter Allgemeine limezungumzia maandamano katika miji kadhaa ikiwa ni pamoja na Kisangani na mji mkuu Kinshasa dhidi ya serikali.

Wer hat das Bild gemacht/Fotograf?: DW/ Simone Schlindwein Wann wurde das Bild gemacht?:20.11. 2012 Wo wurde das Bild aufgenommen?: Goma Ostkongo Bildbeschreibung: Bei welcher Gelegenheit / in welcher Situation wurde das Bild aufgenommen? Wer oder was ist auf dem Bild zu sehen? Polizisten müssen zur M23 überlaufen

Goma Kongo Polizei im Stadion

Gazeti la Die Tageszeitung linazungumzia jinsi maelfu ya wanajeshi wa serikali na polisi walivyojiunga na waasi wa M23 mara baada ya mji wa Goma kutekwa."Hawakupigana,wamekimbia M23 walipoingia.Sio wote lakini waliokimbia,wengi walivua sare zao na kujificha kabla ya kuitika mwito wa waasi na kujiunga nao" limeandika gazeti hilo la Die Tageszeitung lililomnukuu luteni kanali Mankesi wa vikosi vya jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo akisema "hawajakua na njia nyengine."

Die Tageszeitung limeripoti pia kuhusu dhamiri za serikali kutopakata mikono.Limenukuu waziri mkuu Matata Ponyo akisema katika taarifa mjini Kinshasa-wataendelea kupigana.Serikali imetuma wanajeshi mashariki ya Kongo na kuna uvumi kumezuka mapambano ya kuania uongozi jeshini,linaandika die Tageszeitung.Juhudi za kidiplomasia pia zimeshika kasi,rais Kabila anasemekana amekubali wakati wa mkutano wa Kampala pamoja na rais Paul Kagame wa Rwanda na rais Yoweri Museveni wa Ugandakuzungumza na M23 ikiwa wataacha "uvamizi.

***Achtung: Nur zur mit Kevin Gentjes abgesprochenen Berichterstattung verwenden!*** Djatou Touré, Sängerin von der Elfenbeinküste eingestellt im Juli 2012

Djatou Touré Sängerin

Mada nyengine iliyozingatiwa na wahariri wa magazeti ya Ujerumani inahusu haki za wakinamama nchini Côte d'Ivoire.Lilikuwa gazeti hilo hilo la mjini Berlin,die Tageszeitung lililozungumzia pia mzozo ulioitikisa serikali ya muungano ya rais Alassane Ouattara.Mzozo huo umesababishwa na mageuzi ya sheria zinazowapatia wakinamama haki sawa na wenzao wa jinsia ya kiume.Rais Alassane Ouattara alilazimika kuivunja serikali na kuunda mpya lakini wadadisi wanahisi sheria ya haki sawa ni kisingizio tu.

Projekt: Jagd auf Rohstoffe Infografik Exporte Mosambik Nigeria brasilianisch

Infografik Exportações totais de Moçambique em 2011

Mada yetu ya mwisho magazetini hii leo inahusu matumaini yanayowekewa bara la Afrika.Bara la Afrika kwa miongo kadhaa lilikuwa likiangaliwa kama bara lisilokuwa na matumaini yoyote:Hivi sasa lakini "neema ya mali ghafi,mageuzi ya kisiasa na kizazi kipya cha viongozi vijana wa kiafrika waliopania kuziongoza nchi zao kuelekea ulimwengu wa utandawazi ndio sababu ya matumaini hayo",linaandika gazeti la Handelsblatt linalozungumzia makosa yaliyofanyika miaka 50 iliyopita,pale benki kuu ya dunia ilipoashiria mustakbal mwema wa kiuchumi kwa mataifa ya Afrika kusini mwa jangwa la Sahara.Ukuaji wa kiuchumi ulikadiriwa kupindukia ule wa Asia na kufikia asili mia 7 kwa mwaka.Kilichotokea lakini ni chengine;Katika wakati ambapo nchi za Asia,zikitanguliwa na Japan na China zilikuwa zikinyemelea mataifa ya kiviwanda ,Afrika ilididimia katika mtafaruku,badala ya ukuaji wa kiuchumi,Afrika ilizongwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe,njaa,Malaria na Ukimwi.Hali imebadilika,tangu mwaka 2000 uchumi wa Afrika unakuwa haraka kupindukia eneo lolote lile la dunia. Mnamo miaka ijayo shirika la fedha la kimataifa linategemea ukuaji wa kiuchumi wa Afrika kuongezeka kwa asili mia tano kwa mwaka.

.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/ALL PRESSE

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman