1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kutafuta habari kwenye Mtandao – Teknolojia mpya ya Habari

28 Aprili 2011

Kwa wengi, ulimwengu sasa umekuwa kama kijiji. Watu wanawasiliana kupitia barua-pepe, mitandao ya kijamii au hata simu za mkononi. Noa Bongo inapigia mbizi suala la Teknolojia ya kisasa ya mawasiliano Ulimwenguni.

https://p.dw.com/p/MD74
Waafrika wengi zaidi wameunganishwa na mtandao wa mawasiliano wa intanetiPicha: LAI F

Je wewe huwasiliana na jamaa zako nchini Marekani?  Je umewahi  kutoa maelezo yako mafupi kwenye mtandao wowote wa kijamii? Au je, hutumia mtandao wa Intaneti kufanya utafiti wa kazi zako?

Katika sehemu nyingi Barani Afrika, ukosefu au huduma duni  na za pole pole za mtandao wa Intaneti bado ni kikwazo na tatizo kubwa kwa watumiaji wake. Lakini sasa bara hili limo mbioni kurekebisha hali hii.

Teknolojia mpya ya mawasiliano inakupa  fursa nzuri ya kuboresha maisha yako kupitia huduma hizi na hasa kwa wanaotumia simu za mkononi ambazo zimerahisisha sana mawasiliano. Lakini  teknolojia hii mpya pia inakuja na changamoto zake.

Na hii ndio sababu Noa Bongo inajaribu kulipigia mbizi suala hili ili kutoa mwangaza zaidi kuhusu matumizi  ya teknolojia hii mpya. Kupitia mchezo wa  redio, tunasikia hadithi kuhusu  kundi la vijana wanaoamua kijitosa katika biashara ya kutoa  huduma za teknolojia hii mpya ya mawasiliano. Sikiliza upate kufahamu  masaibu yanayowakumba baada ya kuanzisha mkahawa wao wa kutoa huduma hizi za intaneti.

Vipindi vya “Learning by Ear” ‘Noa bongo Jenga Maisha yako, vinasikika katika lugha sita ikiwa ni lugha ya Kiingereza, Kifaransa, Kiswahili, Kihausa, Kireno na Kiamharik. Na vinafadhiliwa na wizara ya mambo ya nchi za kigeni ya Ujerumani.