Kusini mwa Irak sasa kwaripuka | Matukio ya Kisiasa | DW | 11.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Kusini mwa Irak sasa kwaripuka

Eneo la kusini mwa Irak kandoni mwa Basra llikuwa kwa kadiri fulani ni shuwari na washia wengi huko wakishirikiana na watawala.sasa mambo yamegeuka wanadai majeshi ya kigeni yan'gatuke na wachoma moto bendera ya Marekani.

Wairaki waishio kusini mwa nchi hii, wakionekana kushirikiana na vikosi vinavyoikalia Irak kwa kadiri wakiungamkono hatua za kiutawala zilizochukuliwa na serikali kadhaa zilizofuatia kuangushwa kwa utawala wa Saddam Hussein.

Sehemu kubwa ya wakaazi kusini mwa Iraq ni waislamu wa madhehebu ya shia na Iraq imekuwa na serikali yenye washia wengi ingawa chini ya hali ya kukaliwa.

Maandamano makubwa ya hivi majuzi dhidi ya vikosi vya Marekani yalioingiza maalfu ya washia huko Najaf ,Kut na miji mingine ya kusini mwa Irak,yamebainisha kugeuka kwa sura ya mambo na kutoka siasa ya kushirikiana nayo sasa wanapambana nayo.

Waandamanaji huko waliodai kukoma kukaliwa na majeshi ya kigeni yanayoongozwa na Marekani,walichoma moto bendera ya Marekani na kupaza sauti ‘kifo kwa Marekani.”.

Brig.Jenerali Abdul Karim al-Mayahi,kamanda wa polisi mjini Najaf aliwaambia maripota kwamba si chini ya umma wa watu nusu-milioni walishiriki katika maandamano hayo.

Luteni-Col.Christopher Garver,msemaji wa majeshi ya Marekani mjini Baghdad, aliwaambia maripota, “Tunasema tupo hapa kusaidia demokrasia.Tunasema uhuru wa kujieleza na wa kujumuika, ni sehemu ya demokrasia hiyo.Wakati hatukubaliani na risala inayotoka kwenye maandamano hayo, tunakubaliana na haki ya kujieleza.”

Mapigano kufuatia maandamano hayo yaliacha alao askari mmoja wa kimarekani ameuwawa na mwengine amejeruhiwa huko Diwaniyah,km 180 kusini mwa Baghdad.

Mapigano yakiendelea huko Diwaniyah baian ya vikosi vinavyoikalia Irak na vile vya wanamgambo wa Mehdi chini ya uongozi wa imam wa kishia Muqtada al-Sadr.Vikosi zaidi vya kuimarisha hali ya mambo vya kimarekani na vya kiiraq, vikapelekwa huko kuwatia nguvuni na kusaka nyumba hadi nyumba, iwapo kuna silaha au wanamgambo wanaotafutwa.Hadi sasa mwezi huu,askari 5 wa kigeni wnaoikalia Iraq, wamekuwa wakiuwawa kila siku kwa kipimo cha wastani.

Miaka 4 ya kukaliwa Iraq imejionea mageuzi mengi katika mikakati ya majeshi ya Marekani-tangu kubadilishwa kwa mabalozi hata kwa mbinu,lakini mageuzi hayo pengine ni machache na yaliokawia mno.Col.wa zamani wa kikosi cha Polisi cha Iraq Ahmed Jabbar, amenungunika kuwa kuchelewa mno kufanya mabadiliko ya kisiasa, kumeigharimu Iraq,Marekani na dola nyengine gharama kubwa.Mtu aweza alao kusema, dunia ilikua bora zaidi kwa wairaki bila ya kukaliwa na majeshi ya kigeni pamoja na kuwapo ukosefu mkubwa wa usalama.

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com