1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kushughulikia maiti

Kriesch, Adrian5 Desemba 2014

Maiti za watu waliofariki kutokana na Ebola bado zina uwezo wa kusambaza virusi, hivyo mtu hapaswi kuzishika maiti hizo

https://p.dw.com/p/1DzfK
Sierra Leon Ebola Beerdigung Opfer 14.08.2014
Picha: AFP/Getty Images

Maiti za watu waliofariki kutokana na Ebola bado zina uwezo wa kusambaza virusi, hivyo mtu hapaswi kuzishika maiti hizo. Katika mataifa ya Afrika Magharibi, watu wengi wameambukizwa virusi vya Ebola kwa kuzingatia zaidi mazishi ya kitamaduni, kupigana busu, kuosha au kushika maiti. Ni muhimu kujiepusha kushika maiti za waathiriwa wa Ebola.

Godoro, nguo na vitu vingine vilivyotumiwa na mgonjwa vinapasa kuchomwa ili kuzuia kusambaa kwa virusi.

Na shughuli za maziko zinapasa kufanywa na watu waliopewa mafunzo. Katika mataifa ya Guinea na Sierra Leone, Shirika la Msalaba Mwekundu limetoa mafunzo maalum kwa makundi ya wahudumu ambao huitwa kupitia laini ya simu ya dharura kufanya shighuli hii ya maziko. Maafisa hawa hutoa vifaa maalum kama vile mifuko ya plastiki inayotumiwa kuzika maiti, badala ya jeneza la mbao kama ilivyo desturi au hata maiti hizo kuchomwa kabisa. Ingawa ni muhimu kuwa na tahadhari wakati wa kushughulikia maiti, pia ni muhimu maiti hizo kupewa heshima zinazostahilli, na wahudumu wa afya wamepewa mafunzo ya jinsi ya kuwazika kwa heshima zote za Kiislamu na Kikristo watu wanaofariki kutokana na Ebola.