Kurejeshwa kwa wapiganaji wa FDLR Rwanda | Matukio ya Kisiasa | DW | 01.08.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Kurejeshwa kwa wapiganaji wa FDLR Rwanda

Nchini Kongo wapiganaji 67 wa kundi la waasi la FDLR wamejisalimisha kwenye kambi ya Masiki eneo la Mashariki.Shughuli hiyo ilifanyika hapo jana mkoani Kivu ya Kaskazini.

default

Mwanajeshi wa Umoja wa Mataifa nchini Kongo

Ujumbe wa Umoja wa mataifa nchini Kongo MONUC ulio mkubwa zaidi ulimwenguni umekuwa ukihusika na shughuli ya kuwarejesha kwao Rwanda wapiganaji hao wa FDLR.Itakumbukwa kuwa mwaka 2005 kundi hilo la FDLR lilitangaza kuwa linataka kurejea nyumbani kwao Rwanda vilevile kusitisha mapigano.Tamko hilo lilitolewa mjini Roma nchini Italia chini ya upatanishi wa jamii ya Sant'Egidio.

John Kanyunyu alihudhuria shughuli hiyo na kututumia taarifa ifuatayo.
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com