1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kura zahesabiwa Sierra Leone

9 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBRJ

SIERRA LEONE:

Kura zinaendelea kuhesabiwa nchini Sierra leone kufuatia uchaguzi wa jana wa uarais kati ya watetezi wawili wa usoni kabisa Ernest bai koroma wa chama cha All Peoples Party (APC) na makamo-rais Solomon Berewa wa chama-tawala cha Sierra leone Peoples party.

Utaratibu wa kuhesabu kura unasimamiwa na waakilishi wa vyama hivyo,pamoja na wachunguzi kutoka nchini na nje ya Sierra leone.Matokeo yanatazamiwa kutangazwa na Tume ya Uchaguzi mnamo wiki 2 zijazo.