Kura ya maoni yapigwa Zanzibar na Pemba | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 31.07.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Kura ya maoni yapigwa Zanzibar na Pemba

Wananchi visiwani Unguja na Pemba leo wanapiga kura ya maoni kuamua iwapo kuundwe serikali ya umoja wa kitaifa ili kumaliza migogoro ya mara kwa mara kuhusu uchaguzi visiwani humo.

Ras Nungwi village is famous for wonderful beaches and for his shipyards, Insel Zanzibar, Tansania

Pwani maarufu ya kijiji cha Ras Nungwi kisiwani Zanzibar.

Chama tawala cha CCM na chama kikuu cha upinzani cha CUF, vinaunga mkono kura hiyo ya maoni na vimetoa mwito kwa wananchi kuipigia kura ya "ndio."

Kuambatana na muundo mpya wa serikali hiyo, Zanzibar itakuwa na rais alie na makamu wawili. Makamu wa kwanza wa rais atatoka katika chama kitakachoshika nafasi ya pili katika uchaguzi na makamu wa pili atatokea chama kitakachoshinda.Mawaziri watachaguliwa kwa kuzingatia misingi ya uwiano.

Iwapo kura hiyo itapitishwa,katiba ya Zanzibar itafanyiwa marekebisho, ili kufungua njia ya kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa kwa matayarisho ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanywa Oktoba 31 mwaka huu wa 2010.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com