1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kura ya Kombe la mashirikisho Johannesberg

21 Novemba 2008

Kura ya kombe la Confederations Cup kabla kombe la dunia 2010 yapigwa leo.

https://p.dw.com/p/FzFx
Bayer Leverkusen (nyekundu) yatamba bado.Picha: picture alliance/dpa

Baada ya changamoto za timu za Taifa kati ya wiki-Ujerumani ikizabwa mabao 2:1 na mahasimu wao Uingereza,Argentina chini ya kocha mpya Maradona ikiitoa Scotland kwa bao 1-0,macho mwishoni mwa wiki hii yanakodolewa Afrika kusini ambako mbele ya warembo wa dunia wanaoania taji mwezi ujao la mrembo kabisa wa dunia"Miss World",kura inapigwa leo mjini Johannesberg juu ya jinsi timu zitakavyopambana Juni mwakani kwa Kombe la mashirikisho-Confederations Cup-kombe linalofungua pazia la Kombe la Dunia,2010.Leo pia ni finali ya Confederations Cup kati ya klabu 2 za Afrika Etoile du Sahel ya Tunisia na mabingwa watetezi wa kombe hilo CS Sfaxien pia ya Tunisia.

Macho basi yanakodolewa leo Johannesberg,Afrika kusini, ambako homa ya kombe lijalo la dunia 2010 ilianza tangu mwishoni mwa wiki iliopita ilipoanza count-down-kuhesabu siku hadi kombe la kwanza la dunia barani Afrika litakapofunguliwa 2010.Leo kura inapigwa mbele ya warembo 8 watakogombea mwezi ujao taji la mrembo wa dunia-"Miss world".Warembo hao watamsaidia Katibu mkuu wa FIFA-shirikisho la dimba ulimwenguni Jarome Valcke, kuongoza kura hiyo ya timu 8 zitazowakilishja mabara na kanda mbali mbali za dimba ulimwenguni Juni mwakani.

Timu hizo 8 ni Misri,inayowakilisha Afrika kama mabingwa wake ;Brazil -mabingwa wa Amerika kusini,Itali mabingwa wa dunia,Spain,mabingwa wa Ulaya,Marekani mabingwa wa Amerika kaskazini ,Irak mabingwa Asia na New Zealand ikiwakilisha eneo la Concacaf pamoja na wenyeji Afrika kusini.

Leo pia ni finali ya kombe kama hilo kwa klabu za Afrika-Kombe la CAF-African Confederations Cup:Klabu 2 za Tunisia zinaania taji hilo-mabingwa watetezi CS Sfaxien na Etoile du Sahel.Kwa kila hali kombe litasalia Tunisia.Kocha wa Sfaxien ana matumaini makubwa kuwa kombe leo litakuwa lao ingawa duru ya kwanza ya finali hii ilimalizika sare 0:0.

Katika Ligi barani Ulaya, Bundesliga inarudi uwanjani huku macho yakikodolewa mjini Cologne ambako timu 2 zilizopanda daraja ya kwanza msimu huu zinaumana:Hoffenhiem inaongoza Ligi pamoja na Bayer Leverkusen.Cologne ilipoteza pointi 3 jumapili iliopita huko Bremen na haimudu kutoa pointi 3 nyengine nyumbani hii leo.

Hoffenheim ili kubakia kileleni nayo itachachamaa kuzoa pointi zote 3.Walinzi wa FC Cologne kwahivyo, watakuwa na kibarua kigumu jioni hii kuzima vishindo vya chipukizi wa Hoffenheim. Cologne, ilikua timu pekee iliothubutu kuilaza Hoffenheim mara 2 msimu uliopita wakati timu zote 2 zikicheza daraja ya pili. Hoffenheim kwahivyo, itaingia uwanjani kulipiza kisasi kwa mapigo hayo 2 ya mwaka jana.

Bayer Leverkusen,wana changamoto kali mbele ya Armenia Bielefeld na mpambano huo hautakuwa rahisi kwao.kwani, Leverkusen imeilaza mara 1 tu Bielefeld katika mechi zao 7.Mabingwa Bayern Munich, waliopoteza pointi 2 mwishoni mwa wiki iliopita walipotoka sare 2:2 na Borussia Monchengladbach,wana miadi leo na Energie Cottbus.

Kocha wa Munich Jurgen klinsmann ,anatumai watasahau pigo la mwishoni mwa wiki iliopita na kutamba leo mbele ya Cottbus.Katika Premier League-ligi ya Uingereza, Chelsea na Liverpool kila moja itapania jumamosi hii ili kubakia kileleni:

Ikiwa pointi 8 usoni kutoka Manchester United na tofauti kwa magoli tu na Liverpool, Chelsea ina miadi New Castle huku mahasimu wao Liverpool wana wakaribisha Fulhalm huko Anfield.Chelsea lakini, itabidi kucheza bila jogoo lao la Ivory Coast, Didier Drogba lililofungiwa .Lakini ,hii haitamzuwia mfaransa Nicolas Anelka kutamba kama karibuni.

Liverpool ikicheza nyumbani hadi sasa imepoteza pointi 2 tu nyumbani msimu huu na hii yatoa tamaa ya ushindi.Mabingwa Manchester United wana mtihani mkubwa kuweza kufua dafu mbele ya Aston Villa iliopo nafasi ya 5 kwa ya 3 ya Manchester.