Kundi la G7 lataka majibu kuhusu vita vya Iran
27 Machi 2026
Matangazo
Hayo yamejiri wakati kukiwa pia na wasiwasi wa uhusiano wa Urusi na Jamhuri hiyo ya kiislamu.
Kwa upande wake Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Johann Wadephul amesema Jumuiya ya Kimataifa inahitajika kushirikiana kwa ukaribu zaidi kwa sasa wakati inaposhughulikia vita vya aina mbili, akimaanisha vita vya Urusi na Ukraine ambayvo amedai Urusi na Iran inashirikiana kuvitekeleza.
Kwengineko waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uingereza Yvette Cooper amesisitiza kwamba kundi la G7 lina wasiwasi kuhusu mafungamano ya Urusi na Iran baada ya ya nchi za Magharibi kuituhumu Moscow kuisaidia Tehran kushambulia vituo vya Marekani katika eneo la Ghuba.
Urusi imekanusha vikali tuhuma hizo.