1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kumbukumbu za wahanga wa manazi zafanyika

25 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CxWh

Bunge la Ujerumani leo limefanya kumbukumbu za wahanga wa utawala wa kiimla wa manazi.

Rais wa bunge hilo, Norbert Lammert, amewakumbusha wabunge katika kumbukumbu hizo juu ya uhalifu dhidi ya binadamu na mauaji ya halaiki yaliyopangwa na manazi.

Aidha kiongozi huyo amesisitiza jukumu muhimu la bunge katika vita dhidi ya imani ya kuwapinga wayahudi, ubaguzi wa rangi na kutovumiliana.

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, na rais Horst Köhler walihudhuria kumbukumbu hizo.

Ujerumani itafanya kumbukumbu za kitaifa za wahanga wa mauaji ya halaiki ya wayahudi keshokutwa Jumapili.