Kumbukumbu ya miaka kumi tangu kufariki kwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere | Matukio ya Kisiasa | DW | 14.10.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Kumbukumbu ya miaka kumi tangu kufariki kwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Leo ni miaka 10 tangu kufariki dunia Rais wa kwanza wa Tanzania na mmoja kati ya waliokuwa viongozi mashuhuri barani Afrika Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere wa Tanzania

Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere wa Tanzania

Marehemu Nyerere hata hivyo ameacha maoni ya mchanganyiko kuhusu utawala wake wa kijamaa na msiamamo wake katika masuala ya Afrika na kimataifa. Pamoja na hayo moja kati ya mafanikio yake makubwa ni mchango uliotolewa na nchi yake katika ukombozi wa bara la Afrika .Nimezungumza na Mwenyekiti wa wakfu wa Mwalimu Nyerere Dr Salim Ahmed Salim aliyewahi kuwa Waziri mkuu wa Tanzania na baadae katibu mkuu wa uliokuwa umoja wa nchi huru za Afrika OAU, na kwanza anaelezea jinsi Mwalimu Nyerere anavyokumbukwa .

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com